UEFA YANUKIA KWA ATLETIC BILBAO, YAITANDIKA RAYO VALLECANO 3-0 LA LIGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/uefa-yanukia-kwa-atletic-bilbao.html
KLABU
ya Atletic Bilbao amefufua matumaini ya kucheza ligi ya mabingwa barani
ulaya msimu ujao baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rayo Vallecano
katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania, La Liga usiku huu.
Bilbao
chini ya kocha Ernesto Valverde wameshinda dhidi ya wenyeji wao waliopo
nafasi ya katikati ya msimamo na wameongeza nguvu ya kufuzu UEFA kwa
mara ya kwanza tangu walipomaliza katika nafasi ya pili katika msimu wa
La Liga msimu wa 1997-98.
Mabao
ya kipindi cha kwanza ya Mikel San Jose dakika ya 20 na Oscar de Marcos
katika dakika ya 30 yalionesha upepo mzuri kwa Atletico Bilbao wenye
`Mzuka` mkubwa wa kuonja uhondo wa UEFA mwakani.
Mabao hayo mawili yalisababishwa na kona mbili zilizochongwa kutoka winga ya kushoto na mabeki wa Vallecano kushindwa kuokoa.
Baada
ya bao la De Marcos , mashabiki wa Bilbao waliingia karibu na uwanja
wakiwasalimia wachezaji na kusababisha hofu ya kukosekana kwa usalama.
Lakini
hakuna aliyepata matatizo na morali ya mashabiki wa Bilbao iliongezeka
zaidi kipindi cha pili baada ya Ander Herrera kufunga bao katika dakika
ya 74 kwa mpira wa adhabu ndogo.
Matokoe
hayo yanaifanya Bilbao kuwa mbele kwa pointi 9 dhidi ya timu ya Sevilla
iliyopo nafasi ya tano, huku ikiwa na mechi tatu, lakini haiwezi
kuiondoa Bilbao katika nafasi hiyo kutokana na kuwa dhaifu msimu huu.