MKUTANO WA MWAKA WA BENKI YA AFRIKA-RWANDA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mkutano-wa-mwaka-wa-benki-ya-afrika.html
Mh.Saada
M.Salum akifafanua jambo katika moja ya Mikutano ya Magavana wa Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na watendaji wa mashirika mbalimbali ya
Kimataifa,Kulia kwa Mh.Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha – Dkt.
Servacius Likwelile na Kushoto ni Bwa.Peter Noni Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Rasimali Tanzania (TIB).
Mh.Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa mwaka
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo
uliofunguliwa na Mh.Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini
Kigali Rwanda.
Na Mwandishi wetu, Kigali, Rwanda
Serikali
ya Tanzania ipo imara katika kuendelea na kusimamia juhudi zinazofanywa
na Banki ya Afrika katika kuinua mitaji kupitia mpango wa sita wa
kukuza mitaji wa benki hiyo (GCI-VI).
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akitoa
hotuba yake kwa Magavana wa nchi za Afrika katika mkutano wa mwaka wa
wadau wa Benki ya Afrika jijini Kigali, Rwanda.
Mh.Saada
amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa na uwezo wa
kulipa hisa zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu
ya tatu kwa muda uliopangwa.
Saada
amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa mstari wa mbele
katika kulipa hisa zake zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika
awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Zaidi
ya hayo, Waziri Saada ameendelea kusema kuwa nchi yake imeweza kulipa
hisa zake za awamu ya nne zipatazo kiasi cha Dola za Kimareka 1,279.30
kabala ya muda uliopangwa.
“Ninaamini
ni katika mkutano huu tunaweza kujadili dira ya Benki katika miaka
mingine 50 ijayo kama kauli mbiu ya mkutano huu inavyothibitisha,
“Afrika tunayoitaka miaka 50 ijayo” alisema Waziri Saada.
Aidha,
Waziri Saada alimpongeza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt.
Donald Kaberuka na uongozi mzima kwa kusimamia na kuongoza kwa umahiri
mkubwa majukumu walionayo ya kibenki na kuhakikisha inasonga mbele daima
na kuifanya kuwa benki bora barani humu.
Ili
kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa bara hili lazima kudumisha
ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kijamii na kujipatia maendeleo
endelevu kwa nchi zao na watu wake. Mwaka huu Benki ya Afrika inafikisha
miaka 50 tangu kuasisiwa kwake ambapo imeendelea kuhudumia bara hili
kwa mafanikio makubwa.
Kwa
upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame akifungua mkutano huo alisema
kuwa ili kufikia uchumi wa kati katika Bara la Afrika kwa miaka 50
ijayo inabidi nguvu kubwa ielekezwe kwenye sekta binafsi ambayo
itatengeneza ajira kwa vijana na wanawake.
Mkutano
huo ni wa siku tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu ambapo kabla ya
ufunguzi wa Mkutano huu ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana
ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika
wakiambatana na wajumbe kuwakilisha nchi zao.