MB DOG AIMWAGIA SIFA VIDEO YAKE YA `MBONA UMENUNA`
MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesifia video ya wimbo wake mpya ya Mbona Umenuna akisema imeandaliwa kwa kiwa...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mb-dog-aimwagia-sifa-video-yake-ya.html
MKALI
wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesifia video ya
wimbo wake mpya ya Mbona Umenuna akisema imeandaliwa kwa kiwango cha juu
na kudhihirisha ubora wake.
Mb Dog pichani.
Akizungumza
leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema mashabiki wote
watakaopata bahati ya kuitazama video hiyo iliyotengenezwa na Abby Kazi,
ataamini makali yake.
Alisema
lengo lake ni kuwapatia mashabiki burudani kamili, hivyo wadau wote
wapate muda wa kuitazama video hiyo iliyoachiwa rasmi mwishoni mwa wiki
iliyopita, sambamba na kuingizwa kwenye mitandao ya kijamii, youtube na
blogs.
“Hii
ni safari yangu ya kurudi katika makali yangu ya zamani, hivyo naamini
wimbo wangu ulipokewa kwa shangwe na sasa nimeachia video.
“Mashabiki
wote naomba waniunge mkono kwa kuiangalia kazi hii na kusubiri mambo
mazuri zaidi kutoka kwangu, maana mipango yangu ni kufanya kazi nzuri
zaidi ya Bongo Fleva,” alisema.
Katika
video hiyo, msanii huyo anaonyesha ujuzi wa aina yake wa kuimba, huku
mdundo ‘beat’ yake ikipigwa kisasa zaidi kulingana na mabadiliko ya
kisanii kwa wakali wengi Tanzania.
