Marekani: wanajeshi 80 watumwa Nigeria
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/marekani-wanajeshi-80-watumwa-nigeria.html
Serikali
ya Marekani imewatuma wanajeshi wa ziada nchini Nigeria ili
kushirikiana na wanajeshi wa taifa hilo kwa kuwatafuta wasichana zaidi
ya 200 waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram.
Kundi
hili la Boko Haram linatuhumiwa pia kutekeleza mfululizo wa mashambulizi
katika miji mbalimbali hususan kaskazini na hivi karibuni katika mji wa
Jos katikati mwa nchi.
Wanajeshi
80 wa Marekani wametumwa nchini Chad ili kuendesha “operesheni ya
ujasusi, uchunguzi na ukaguzi katika anga la kaskazini mwa Nigeria na
majimbo jirani”, rais Barack Obama amesema jana jioni katika barua
aliyotumia bunge la taifa hilo.
Wanajeshi hao
watatumia ndege isiyo na rubani ambayo haitokua na silaha yoyote kwa
kufanya ukaguzi na upelelezi katika maeneo yoyote yanayoshukiwa kwamba
wamefichwa wasichana hao, amesema msemaji wa jeshi, kanali Steve Warren,
bila hata hivo ktoa taarifa zaidi kuhusu aina ya ndege hio iliyotumwa.
Idadi hio
ya wanajeshi na vifaa, inaongezwa katika idadi nyingine ya wanajeshi
vifaa viliyotumwa nchini Nigeria tangu juma liliyopita, ikiwa ni pamoja
na ndege zisiyo na rubani, ndege ya ujasusi, na timu nyingi za wataalamu
na washauri ambao wanashirikiana na jeshi la Nigeria katika harakati za
kuwatafuta wasichana hao.
Familia
za watoto hao hazina taarifa yoyote kuhusu wapi walioko watoto zao,
tangu walipotekwa nyara na kundi la wanamgambo wa kislamu la Boko Haram
Aprili 14 mwaka 2014.
Rais wa
Nigeria, Goodluck Jonathan, alitupilia mbali pendekezo liliyotolewa na
kiongozi wa kundi la Boko Hara, Abubakar Shekau, la kubadilishana
wafuasi wa kundi hilo wanaozuiliwa jela na wasichana hao.
Wakati huo
huo Jeshi la Nigeria limeanzisha tangu jumatano wiki hii zoezi la
kusajili watu wanotaka kujiunga na jeshi kwa hiyari yao kwa lengo la
kupambana na kundi la Boko Haram