Mambo bado mabaya! Ule ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga hadi kufika mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza, Risasi Jumatano linakuhabarisha. Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, wakiwa kwenye pozi enzi za ushosti wao. Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani. Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole. Ilisemekana kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini. Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. “Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana, hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya kulumbana,” kilisema chanzo hicho kikikataa kutaja majina ya wabunge hao na kutaka aulizwe Steve. Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao. Kajala Masanja. Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa hao.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mambo-bado-mabaya-ule-ugomvi-wa.html
Mambo bado mabaya! Ule ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga hadi kufika mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza, Risasi Jumatano linakuhabarisha.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, wakiwa kwenye pozi enzi za ushosti wao.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge
hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana
kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge
hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi
tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
“Walimwambia
Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana,
hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha
kushikamana kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya
kulumbana,” kilisema chanzo hicho kikikataa kutaja majina ya wabunge hao
na kutaka aulizwe Steve.
Gazeti
hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye
alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati
ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi
wanatamani kuwa kama wao.
Kajala Masanja.
Risasi
Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema
hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa
hao.


