Flatnews

KINANA SEPUKA



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amebeba Jogoo aliyepewa zawadi na wakina mama wa tawi la UWT Puma,Katibu Mkuu alifungua shina la wakina mama wajasiriamali wanaojishughulisha na kilimo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kuvuna viazi vitamu pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai kwenye shamba la mkulima Bernardo Razalo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Ighombwe ambapo aliwahimiza viongozi wa CCM kujenga ofisi zenye uwezo wa kutoa  msaada wa kijamii ikiwa pamoja na elimu za ujasiriamali.

Wasanii wa kikundi cha ngoma wakicheza ngoma ya Peni wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ofisi za CCM kata ya Ighombwe.


Wasanii wa kwaya kutoka Sepuka wakiburudisha kabla ya kuanza kwa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Sepuka, Ikungi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Sepuka na kuwataka kuungana katika kushiriki kuleta maendeleo hasa yale yanayohusu jamii kama kujenga shule, maabara na zahanati.

Post a Comment

emo-but-icon

item