Flatnews

Iringa na Njombe kukusanya takwimu za sensa ya viwanda

MENEJE TAKWIMU IRINGA/NJOMBE FABIAN FUNDI


SDC10773_0777b.png


MENEJE TAKWIMU IRINGA/NJOMBE FABIAN FUNDI

Iringa/Njombe. Ofisi ya Taifa ya Takwimu hukusanya takwimu na kusambaza machapisho ya taarifa za kitakwimu za kitaifa na kimataifa.

Ofisi hiyo ilifanya zoezi la  Sensa ya Watu na Makazi  mwaka 2012 na machapisho yameanza kutolewa, Watu wote wanakaribishwa kwenye Ofisi zote zilizoko mikoa yote ya Tanzania  ili kuweza kupata taarifa nyingi za takwimu.

Hivi sasa sensa imejikita kufanya takwimu mbili tofauti kwa kipindi hiki ikiwa ni pamoja na Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi ambapo ukusanyaji wa takwimu hizi ulianza tangu mwezi Februari mwaka huu.

Semina ya Wadadisi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwanza na kukamilika tarehe 16 mwezi wa pili lengo ikiwa ni kutoa mafunzo kwa Wadadisi wa kwenda kukusanya takwimu hizo.

Baada ya kukamilika ukusanyaji wa takwimu hizi zitapima mwelekeo wa ajira nchini.

Utafiti wa pili ambao unafanyika kwa hivi sasa ni Sensa ya Viwanda ambayo inafanyika nchi nzima, mafunzo ya Sensa hiyo yalifanyika mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi wa nne na kuhitimishwa tarehe saba mwezi huo huo,hata hivyo zoezi la uorodheshaji wa viwanda linafanyika kwa ngazi ya kata mpaka kijiji.

Fundi aliongeza kuwa zoezi hili la Sensa viwanda linahusisha shughuli kuu nne
1.    Uchimbaji wa Madini, Mawe,      Kokoto na Mchanga
2.    Uzalishaji wa bidhaa.
3.    Uzalishaji na usambazaji wa Umeme, Maji,  GesiMvuke (Steam)
4.    Usambazaji wa maji Safi na Taka
Shughuli zote hizi hufanyika katika maeneo maalumu.

Fundi amesema kuwa mara ya mwisho kufanyika kwa zoezi la Sensa ya Viwanda Tanzania ilikuwa ni mwaka 1990. Kipindi hicho alikuwa mkoa wa Mwanza akiwa kama msimamizi wa zoezi hilo.

Hata hivyo Changamoto ambayo wanakutana nayo katika ukusanyaji wa takwimu ni pamoja na watu kupeleka mtazamo wa Sensa ya Viwanda kisiasa hivyo wananchi wanapaswa kutambua kuwa zoezi ni la Kiserikali, Zoezi lolote la ukusanyaji wa takwimu halihusiani na siasa wala manufaa ya mtu mmoja bali ni kwa faida ya Taifa zima.

”Takwimu zinazopatikana zinapima hali halisi ya maendeleo ya nchi kwa utaratibu wa Serikali inavyojiwekea malengo ya maendeleo.  Kwa mfano malengo ya melinia, Ofisi ya Taifa ya Takwimu hufanya tafiti na kutoa ripoti za tafiti hizo kwa Serikali na wadau wa maendeleo ili kuona kama inafikia malengo iliyojiwekea” Alisema Fundi.

Aidha ameongeza kuwa Takwimu zinakusanywa bure na kutolewa bure kwa Wadau wote wa Maendeleo, Lakini pia ikumbukwe kuwa kulingana na Sheria ya TAKWIMU ya Mwaka 2002 takwimu zinakusanywa na kutunzwa kwa USIRI mkubwa mpaka uchambuzi unapokamilika na kutolewa ripoti ambayo huonyesha idadi au asilimia na haionyeshi jina la mtu au kikundi fulani.

Sensa ya Viwanda inahusisha viwanda vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa,inahusisha pia kuanzia ajira ya mtu mmoja na kuendelea anaweza kuwa ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe kwenye kiwanda hicho, wananchi wakitoa ushirikiano ripoti itakapotoka itatoa ufafanuzi halisi ya viwanda nchini.

Lengo la kufanya Sensa ya Viwanda ni Serikali na Wadau wa maendeleo kuvitambua viwanda vyote nchini, mahali vilipo na kujua ni viwanda vya aina gani ili hata Serikali inapotaka kuviendeleza inajua ni viwanda vya aina ipi na viko sehemu ipi. Lakini pia siyo Serikali peke yake hata Wadau wote wa maendeleo nao watajua ni jinsi ipi kwa kusadiana na Serikali wanaweza kuendeleza kundi lipi la viwanda.

Sambamba na hayo Fundi ametoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kwa sababu takwimu zitakazo patikana ni za wadau wote wa maendeleo kwani mtu yeyote atakayehitaji kupata takwimu za kuhusu viwanda vilivyopo katika kata au kijiji basi Sensa ya viwanda itamsaidia kutambua jumla ya viwanda na vya aina ipi vilivyopo kwenye eneo lake.

Post a Comment

emo-but-icon

item