HOFU YATANDA WASAMARIA WEMA WAINGIA MITINI DHAMANA YA WAZAZI WA MTOTO WA BOKSI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/hofu-yatanda-wasamaria-wema-waingia.html
Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani
hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi ni Rashid Mvungi (47), mama mlezi,
Mariam Said (38) na mume wake Mtonga Omar (30).
Washitakiwa hao walifikishwa katika
mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo, Jumatatu ya
wiki hii na kusomewa mashitaka hayo huku muda mwingi wakionesha kujutia
kosa hilo ambalo hawakujua kama ni bomu ambalo litakuja kulipuka.
Muda mwingi, Mvungi akiwa mahakamani
hapo alikuwa akiweka mikono juu ya kichwa (angalia picha) jambo
lililotafsiriwa kwamba ni kuonesha kujutia tukio hilo.
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera
alisema washitakiwa walitenda kosa hilo kati ya Desemba, mwaka 2010 na
Mei, mwaka huu katika Mtaa wa Azimio Kata ya Kiwanja cha Ndege, mjini
Morogoro.
Wakili huyo alidai kuwa katika
kipindi hicho, washitakiwa wakiwa walezi wa mtoto Nasra, walimfanyia
ukatili wa kumtelekeza na kumpa malezi akiwa ndani ya boksi na hivyo
kumsababishia magonjwa mbalimbali.
Maradhi yaliyotajwa kumkumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi ni utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa mifupa katika mwili.
Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.
Hata hivyo, licha ya dhamana kuwa wazi, hakuna mtu aliyejitokeza kuwadhamini washitakiwa hao hivyo kurejeshwa gerezani huku watu wakishangilia kwa kusema kwamba kitendo walichokifanya hawastahili kurejea uraiani.
Hata hivyo, licha ya dhamana kuwa wazi, hakuna mtu aliyejitokeza kuwadhamini washitakiwa hao hivyo kurejeshwa gerezani huku watu wakishangilia kwa kusema kwamba kitendo walichokifanya hawastahili kurejea uraiani.