FISI WAKUTWA NA SHANGA NA ROZALI KIUNONI.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/fisi-wakutwa-na-shanga-na-rozali-kiunoni.html
MSAKO
wa Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa
Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.
Maajabu
hayo yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya
12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.
Msako
huo wasiku tatu ulioanza juzi(Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa
Kijiji hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na
Mwang’ombe, wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao 50.
Habari
za ndani kutoka Kijijini humo zimesema kwamba, kabla ya wananchi hao
kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi wanadaiwa kumilikiwa na
watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina, wazee wa Kijiji
na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na nguvu
za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.
