Diego Costa akiwa mjini Belgrade kwa lengo la kuonana na mganga wa kienyeji.
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego
Costa amesafiri kwenda Belgrade nchini Serbia kumuona `Mganga wa
miujiza`, Marijana Kovacevic ili amtibu na kurejea uwanjani haraka kwa
ajili mchezo mkubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Mganga
huyo wa Serbia anawatibu wachezaji wenye matatizo ya misuli kwa
kuwawekea placenta na Costa anataka kuichezea Atletico Madrid kwenye
mechi ya fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid jumamosi ya wiki hii.
Costa
amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya nyama aliyopata wiki iliyopita
kwenye mechi ya mwisho ya ligi kuu nchini Hispania, La Liga dhidi ya FC
Barcelona iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Atletico kufanikiwa kutwaa
ubingwa.

Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade kuonana na mganga wa miujiza, Marijana Kovacevic

Costa (katikati) yuko hatarini kukosa mechi ya fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid.
Majeruhi aliyonayo Costa kwa sasa siku
zote humfanya mchezaji akae nje ya uwanja kwa siku 15 na kama hatapata
nafuu, basi atakosa mechi ya Lisbon.
Kovacevic aliwahi kuwatibu wachezaji
wengi wa ligi kuu akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Asernal Robin van
Persie na kiungo wa Chelsea, Frank Lampard.