EMMANUEL ANORD OKWI ALAMBA MILIONI 10 KWA SAA YANGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/emmanuel-anord-okwi-alamba-milioni-10.html
Imechapishwa mei 23, 2014, saa 6: 36 mchana
STRAIKA, Emmanuel Okwi ameichezea Yanga dakika 687 kwenye mechi nane kwa msimu ulioisha na kuzoa kitita cha Sh120 Milioni sawa Sh 10 Milioni kwa kila saa moja aliyochezea klabu hiyo ya Jangwani ndani ya jezi namba 25.
STRAIKA, Emmanuel Okwi ameichezea Yanga dakika 687 kwenye mechi nane kwa msimu ulioisha na kuzoa kitita cha Sh120 Milioni sawa Sh 10 Milioni kwa kila saa moja aliyochezea klabu hiyo ya Jangwani ndani ya jezi namba 25.
Fungu
hilo linahusisha mishahara na dau la usajili. Katika miezi hiyo minne,
amefunga mabao matatu tu.
Lakini
mabao hayo hayakuwa na madhara chanya kwa Yanga kwani mawili alifunga Yanga
ikiwa imeshinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Ligi na moja aliifunga
Simba iliposhinda mabao 3-1 kwenye Mtani Jembe.
Mabao
ya mchezaji huyo ambaye imeanza kudaiwa kwamba anafikiria kuvunja mkataba na
Yanga kutokana na ushawishi wa wagombea wa Simba hayakuipa Yanga faida yoyote
zaidi ya kuongeza idadi.
Okwi
ambaye sasa yupo katika mgogoro na Yanga akitaka amaliziwe fedha zake za
usajili, ameichezea klabu yake mechi hizo huku akikosa nyingine saba kwa sababu
mbalimbali ikiwemo kugoma na kukosa kibali.
Nyota
huyo aliyeanza kibarua chake Yanga mwishoni mwa mwaka jana baada ya kusaini
mkataba wa miaka miwili na nusu, ameichezea Yanga kwa dakika 687 (Sawa na
michezo nane) ambazo ni mechi za Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika
lakini akaunti yake ikafurika Sh120 Milioni.
Kati
ya Sh120 Milioni alizolipwa Okwi, Sh 96 Milioni alilipwa kama sehemu ya ada
yake ya usajili alipojiunga na Yanga lakini Sh. 24 Milioni alilipwa kama
mshahara wake kwa miezi minne aliyocheza kabla ya kugoma akishinikiza
kumaliziwa kulipwa fedha zake za usajili.
Kwa
mwezi Okwi analipwa dola 4,000 ambazo ni zaidi ya Sh. 6 Milioni hivyo kwa miezi
minne alilipwa Sh. 24 milioni. Okwi alisajiliwa kwa dau la dola 100,000 ambazo
ni zaidi ya Sh. 160 Milioni, lakini Yanga ilimlipa kianzio cha dola 60,000
(Sh96 Milioni) hivyo sasa anaidai dola 40,000 zilizobaki.
Mechi
alizoichezea Yanga ni sita za ligi kuu ambazo ni dhidi ya Ruvu Shooting, Mtibwa
Sugar, Azam FC, Rhino Rangers, Prisons (hakucheza dakika zote tisini) na Mgambo
JKT, wakati kwa upande wa michezo ya kimataifa amecheza mechi mbili nyumbani na
ugenini dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kutokana
na kibali chake kuchelewa kuwasili nchini, Okwi alikosa mechi tatu za mwanzo za
mzunguko wa pili wa ligi kuu ambazo ni dhidi ya Ashanti United, Coastal Union
na Mbeya City. Mechi nyingine aliokosa Okwi ni dhidi ya Komorozine de Domoni ya
Comoro iliyokuwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pia
straika huyo aligomea michezo ya mwisho ya ligi hiyo dhidi ya Simba, JKT
Oljoro, JKT Ruvu na Kagera Sugar.
Ukiachana
na mechi hizo nane za michuano mbalimbali, Okwi aliichezea Yanga mechi ya
kwanza dhidi ya Simba Desemba mwaka jana mchezo maalumu wa kirafiki uliopewa
jina la Nani Mtani Jembe, pia alicheza mechi nne za kirafiki walipokuwa kambini
Uturuki.
Rekodi
zinaonesha kuwa tangu Okwi aondoke Simba mwaka 2012, amecheza jumla ya michezo
14 tu za kimichuano kwenye nchi tatu tofauti za Tunisia, Uganda na Tanzania.
Aliichezea mechi mbili Etoile Du Sahel ya Tunisia, akacheza nne Uganda akiwa na
SC Villa na nane akiwa na Yanga.
Akiwa
Tunisia Okwi aliichezea mechi mbili Sahel akitokea benchi lakini hakuweza kuwa
na maisha mazuri kwani aliachana na timu hiyo na kutimkia Uganda alipocheza
mechi nne za Ligi Kuu ya Uganda baada ya kutokea matatizo ya malipo yake.
Kwa
sasa Okwi yupo Uganda huku majaliwa yake katika kikosi cha Yanga yakiwa shakani
kwani mwenyewe anadai amaliziwe fedha zake za usajili lakini uongozi unamtaka
ajieleze kwa nini amegoma kuichezea timu hivyo unapanga kumkata sehemu ya fedha
zake za usajili.
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji (pichani) amesisitiza kwamba kwavile mchezaji huyo
haikutumikia Yanga ipasavyo lazima wakae mezani wajadiliane mambo mawili
aongeze mkataba mpaka kufikia miaka mitatu au wamkate kiasi cha fedha
anazoidai.
Lakini
mwanasheria wake, Edgar Aggaba amejibu kwamba hakuna kitu kama hicho, Manji
anapaswa kulipa dau walilokubaliana halafu wakae mezani wazungumze mengine.
Chanzo: Mwanaspoti
