CASTLE LAGER PERFECT SIX NGAZI YA MIKOA YAANZA KUTIMUA VUMBI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/castle-lager-perfect-six-ngazi-ya-mikoa.html
Mchezaji
wa timu ya Baracuda, Jamhuri Kihwelo akifunga goli dhidi ya Nato ya
Ukonga kwenye mechi ya nusu fainali iliyofanyika kwenye uwanja Rova
Ashanti Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwenye mashindano ya ‘Castle
Perfect Six’ ngazi ya mikoa ambapo washindi watapata fursa ya kwenda
kuiona timu ya Barcelona, Mashindano hayo yamedhaminwa na bia ya Castle
Lager. Nato ilishinda kwa 5-1.
Meneja
Mradi wa Bia ya Castle Lager, Willhard Malimbo kulia akiwakabidhi
zawadi wachezaji wa Timu ya Gaddafi walioibuka washindi wa kwanza katika
bonanza la Castle Perfect (6) lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe
Yanga Dar es Salaam jana.
Mchezaji
wa Timu ya, Aman kushoto akijalibu kumtoka mchezaji wa timu ya Gaddafi,
Evens David wakati wa mchezo wa fainali ya Bonanza Castle Lager Perfect
6 lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam Gadaffi
ilishinda kwa goli moja kwa bila na kuibuka washindi.
Afisa
Mauzo TBL Kanda ya Kinondoni,Kelvin Kabengula (kulia) akimkabidhi
zawadi nahodha wa timu ya AUCT,Kimala Douglas baada ya timu hiyo
kufanikiwa kutinga hatua ya fainali katika mashindano ya Castle Lager
Perfect Six wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika kwenye uwanja wa CCM
Mwinjuma jijini Dar es salaam jana (Picha: Executive Solutions)
Wachezaji
wa timu ya Infinity Communicatios,wakifurahi baada ya kufanikiwa
kutinga hatua ya Fainali,katika mashindano ya Castle Lager Perfect Six
wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Mwinjuma jijini
Dar es salaam jana (Picha: Executive Solutions)

Na Mwandishi Wetu
Imechapishwa Mei 25, 2014 saa 1: 54 mchana
Mashindano ya Castle Lager Perfect Six ngazi ya mikoa yameanza
kutimua vumbi wikendi hii ambapo jumla ya timu 48 zimeshuka dimbani
katika mikoa ya Dar na Morogoro zikiwania nafasi ya kufuzu kushiriki
ngazi ya kanda na hatimaye fainali za kitaifa.
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo alisema kuwa mechi
zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko
na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa
wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo ya kwanza.
Mechi zilizochezwa wikendi hii ilikuwa ni awamu ya kwanza ya
mashindano hayo ambapo timu zitakazofuzu hatua hiyo ya mikoa zitachuana
katika ngazi ya kanda na hatimaye taifa. Washindi wa fainali za taifa
watajipatia fursa ya kipekee kwenda kutembelea jiji la Barcelona huko
Hispania na kuiona timu ya Barcelona ikicheza na pia wataweza kujionea
mambo mbalimbali ya kihistoria katika uwanja wa Camp Nou.
Baadhi ya maeneo na timu zilizoshiriki ni Ilala ambapo timu
zilizoshiriki ni Nato FC, Gaddafi FC, Barafu Veterani, Pata Habari, Dira
ya Mtanzania, Hazard Team, Mburahati Veterans na Baracuda FC ambapo
mechi hizo zilipigwa kwenye uwanja wa Rova Ashanti na Baracudda FC
waliibuka washindi. Temeke ni Lumo FC, Sunset FC, Flamingo FC, Yombo
Classic, Wazee wa Povu FC, Shelly FC, Mwisho wa Lami FC, na Oilcom FC
ambapo mechi hizo zilipigwa kwenye uwanja wa Mwembeyanga na Gaddafi
kuibuka washindi. Kwa mechi iliyochezwa uwanja wa Mwinjuma Kinondoni
timu ya AUCT iliibuka washindi. Fainali za kanda ya Dar es salaam
zitachezwa Juni 8 kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe ambapo timu
zilizofuzu Temeke, Ilala na Kinondoni zitachuana kupata washindi
watakaoshiriki fainali za taifa.
Na huko Morogoro, timu za soka za Mzinga FC na Ndezi FC
zimefanikiwa kutinga hatua ya fainali za kanda ya mashariki baada ya
kufanya vizuri mashindano hayo yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi
Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika
kwa michezo iliyoshirikisha timu nane mjini hapa, Mwamuzi wa mchezo huo
Elly Sasii alisema kuwa ni timu za Mzinga na Ndezi ndizo zilizofanikiwa
kutinga hatua ya fainali za kanda ya mashariki ikisubiri washindi
wenzao wa mkoa wa Dodoma.
Sasii alisema kuwa Mzinga na Ndezi zitacheza ligi ndogo ya
mashindano hayo Juni 7 mwaka huu Manispaa ya Morogoro na washindi wa
Dodoma ili kupata timu moja itayowakilisha kanda ya mashariki katika
mashindano ya taifa yatayofanyika baadaye jijini Dar es Saalaam.
“Haya mashindano hapa nchini ni mapya na lengo lake ni kupata
timu moja itayoenda Hispania kushuhudia michezo ya Barcelona.”alisema
Sasii.
Sasii alifafanua kuwa washindi hayo walifanikiwa kushinda timu
nyingine katika hatua ya mtoano, robo fainali ikihusisha timu za
Misufini A na B, Nyumbani Park A na B, Airport Rangers na Mtazamo zote
za Manispaa ya Morogoro.
Kanda zitakachuana ni pamoja na kanda ya mashariki, Kaskazi,
kanda ya Ziwa na kanda za nyanda za juu kusini ambapo baadhi ya kanda
michuano hiyo tayari zimeanza rasmi mei 24 mwaka.