ANCELOTTI KOCHA WA PILI KUTWAA `NDOO` YA UEFA MARA TATU, AWAPIGIA `SALUTI` WACHEZAJI WAKE KWA KUMWANDIKIA HISTORIA SAFI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/ancelotti-kocha-wa-pili-kutwaa-ndoo-ya.html

Carlo Ancelotti amekuwa kocha wa pili kushinda makombe matatu ya Ulaya
Mshindi: Ancelotti pia alishinda makombe mawili akiwa na AC Milan mwaka 2003 na 2007.
Imechapishwa Mei 25, 2014, saa 4:00 asubuhi
Carlo
Ancelotti amewapigia `Saluti` na kuwashukuru wachezaji wake baada ya kumuweka katika historia.
Kocha huyo raia wa Italia anakuwa kocha wa pili kushinda makombe matatu ya Ulaya kama alivyofanya Bob Paisley.
"Tulikuwa tunauwazia usiku huu (jana)
tangu mchezo wa kwanza wa msimu huu na hatimaye tumefanikiwa kwa kile
tulichopanga kufanya mwanzoni mwa kampeni". Alisema Ancelotti.
Ancelotti alionekana kuchanganyikiwa
na mchezo huo, lakini mabadiliko aliyoyafanya kwa kumuingiza Isco na
mfungaji wa bao Marcelo yaliwaamusha Real Madrid na kupata ushindi
uliowapa historia ya pekee katika michuano ya ligi ya mabongwa.