Jeshi halijafika gwoza baada ya wiki 2
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/jeshi-halijafika-gwoza-baada-ya-wiki-2.html
Ni wiki nane tangu wasichana 200 watekwe nyara kutoka shuleni mwao kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram
limeimarisha mashambulizi yake kufuatia milipuko ya mabomu katika miji
kadhaa na vijiji.Juma lililopita vijiji kadhaa vilivyoko karibu na mpaka na Cameroon vimeshambuliwa huku mamia ya raia wakiuawa.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja amezungumza na baadhi ya raia ambao wamevitoroka vijiji katika eneo la Gwoza lililopo katika jimbo la Borno,na sasa wamejificha katika eneo la Milima la mandara karibu na mpaka wa Cameroon.
Wanasema kuwa juma moja baada ya shambulizi la wanamgambo wa boko haram hakuna ishara ya wanajeshi wa serikali katika eneo hilo.
Jeshi ladaiwa kutelekeza wakaazi Gwoza jimbo la Borno
Kwa sasa wanalala hadharani katika maeneo ya milima hiyo.
Watu walioachwa bila makao wanasema kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameweka bendara nyeupe na nyeusi za jihad katika vijiji kadhaa na kwamba ni hatari kwa raia kufika katika sehemu hizo.
Serikali ya Nigeria imeonekana kujivuta katika kukiri mashambulizi hayo huko Gwoza eneo ambalo sasa ni makao makuu ya Boko haram.