CRISTIANO RONALDO AWASHA MOTO REAL MADRID IKIINYUKA MANCHESTER CITY
Mbele ya mashabiki 100,000 katika uwanja Melbourne Cricket, Australia kulikuwa na burudani ya aina yake kati ya Manchester City na Re...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/cristiano-ronaldo-awasha-moto-real.html
Mbele
ya mashabiki 100,000 katika uwanja Melbourne Cricket, Australia
kulikuwa na burudani ya aina yake kati ya Manchester City na Real
Madrid.
Vijana wa Manuel Pellegrini leo wamekufa 4-1 dhidi ya vijana wa Rafa Benitez.
Mwanasoka
bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo ametupia goli moja dakika ya 25, huku
Karim Benzema akifunga dakika ya 21, Pepe dakika ya 44 na
Denis Cheryshev dakika ya 73 .
Bao la kufutia machozi kwa Manchester City limefungwa dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti na Yaya Toure.
Kuelekea
katika mechi hiyo, Toure alisema Man City inahitaji kupunguza pengo
lake na Real Madrid pamoja na FC Barcelona katika uwezo wa kusakata
kandanda, lakini kwa ushahidi huu pengo limezidi kuwa kubwa.

Ronaldo akiifungia Real Madrid bao baada ya kumzidi maarifa beki wa Man City Aleksandar Kolarov

Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (katikati) akijiandaa kupiga mpira, huku kipa wa Real Madrid, Keylor Navas akiokoa

Toure alikuwa chini ya ulinzi wa Navas na Sergio Ramos

